FDLR WATOA VITISHO KWA WAJUMBE WA MASHIRIKA YA KIRAIA

FDLR WATOA VITISHO KWA WAJUMBE WA MASHIRIKA YA KIRAIA

Like
210
0
Thursday, 19 March 2015
Global News

WAJUMBE wa Mashirika ya Kiraia wa vijiji vya Tama na Itala Kusini mwa tarafa ya Lubero Jimboni Kivu Kaskazini, wametishwa na kundi la Waasi wa Kihutu kutoka Rwanda-FDLR wanaoongozwa na Kanali KIZITO.

Vitisho hivyo vimekuja kutokana na uchapishaji wa Ripoti ya Mashirika ya Kiraia katika Sekta hiyo.

Baadhi ya Wanachama wa Vyama vya Kiraia katika Vijiji vya Tama na Itala wamesema, raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali ya maficho kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi wanaoishi maeneo hayo hasa FDLR huku wakisema wanaishi kwa tabu huku wakilala usiku misituni.

 

Comments are closed.