FERNANDO ALONSO KUFANYIWA VIPIMO TENA BAADA YA AJALI

FERNANDO ALONSO KUFANYIWA VIPIMO TENA BAADA YA AJALI

Like
282
0
Monday, 23 February 2015
Slider

 Dereva wa kampuni ya magari ya McLaren Fernando Alonso anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi siku ya jumatatu kabla timu ya madaktari wanaomuhumia hawajaamua kama watamruhusu kutoka hospitali

Fernando Alonso mwenye umri wa miaka 33 amewahi kuchukua ubingwa wa dunia mara mbili kwenye mashindano ya magari.

Kwa sasa dereva huyu yupo kwenye uangalizi mkubwa wa madaktari ambapo amelazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kufuatia ajali aliyopata wakati wa majaribio huko Barcelona siku ya jumapili

Alonso kwa sasa anasumbuliwa na tatizo la kupoteza fahamu kwa muda kufutia mshtuko aliupata baada ya fuvu la kichwa kujigonga wakati wa ajali lakini taarifa kutoka kwenye kampuni ya McLaren zimeeleza kuwa hali yake kiafya inaridhisha kwa sasa.

“Alonso ameweka kitengo cha wagonjwa mahututi katika hali ya kawaida wala si kwamba ana hali mbaya na hakuna sababu ya kuwa na hofu juu ya afya yake” alisema meneja wa derva huyo bwana Luis Garcia Abad wakati akizungumza na vyombo vya habari huko Hispania.

Ajli ilikuwa kubwa ila kwa bahati nzuri haikuwa tatizo kwake alikuwa na fahamu pia aliweza kuongea.

Garcia Abad pia amekanusha taarifa zilizokuwa zikidai kuwa Alonso alikuwa akijisikia kizunguzungu kabla ya kupata ajali hiyo.

“nakataa kwamba Fernando alikuwa hayupo sawa kiafya kabla ya kukutwa na ajali hiyo bali ni upepo mkali ulimyumbisha akauvaa ukuta

fff FER

Comments are closed.