Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa limetangaza ubora wa viwango kwa mwezi Agosti ambapo timu ya taifa ya Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza.
Ubelgiji imepanda kwa nafasi moja mpaka nafasi ya pili huku mabigwa wa dunia Ujerumani wakiwa katika nafasi ya tatu.
Timu ya juu kabisa toka Barani Afrika ni Algeria ambayo ipo pale pale Nafasi ya 19 na kufuatiwa na Ivory Coast waliobakia Nafasi ya 21.
Timu za ukanda wa Afrika mashariki zinaongozwa na Uganda walioko nafasi ya 74,Rwanda wakiwa katika nafasi ya 91 Kenya 116,Burundi wakishika nafasi ya 132 na Tanzania wakiwa latika nafasi ya 140
Ifuatayo ni listi ya timu kumi bora duniani kwa mwezi Agosti
Katika viwango hivyo timu yetu ya taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) ipo katika nafasi ya 140 kwa alama moja