FIFA: BLATTER AREJESHA FOMU KUWANIA URAIS

FIFA: BLATTER AREJESHA FOMU KUWANIA URAIS

Like
305
0
Thursday, 29 January 2015
Slider

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Sepp Blatter leo amerudisha fomu za kuwania kugombea urais wa shirikisho hilo kwa awamu ya tano

Kupitia akaunti yake ya Twitter Blatter aliandika

“Today (Thursday) is a key date in the electoral calendar. I’ve made my submission, now the electoral committee follow a process,”

akimaanisha kuwa leo ni siku muhimu katika kalenda ya uchaguzi na amefanya maamuzi hayoya kurudisha fomu hivyo anaichia kazi kamati ya Uchaguzi ifanye kazi yake

alisema Blatter mwenye umri wa miaka 78, ikiwa leo ni siku ya mwisho kwa wagombea kurejesha fomu zao

Blatter ambae amekuwa akishikilia nafasi hiyo toka mwaka 1998, tayari ameonyesha nia yake kuomba kugombea kwa kipindi kingine cha uongozi wa shirikisho hilo la soka duniani na kupata sapoti kubwa kutoka Afrika, Asia n.k

Miongoni mwa wapinzani wake yupo mchezaji wa zamani wa Ureno na Real Madrid mshambuliaji Luis Figo, Michael Van Praag, Ali bin Al Hussein, Jerome Champagne na alikuwa mchezaji wa wa Ufaransa David Ginola.

Comments are closed.