FLOYD MAYWEATHER: DUNIA ITASIMAMA KUSHUHUDIA PAMBANO LANGU

FLOYD MAYWEATHER: DUNIA ITASIMAMA KUSHUHUDIA PAMBANO LANGU

Like
301
0
Thursday, 12 March 2015
Slider

Floyd Mayweather amesema dunia itasimama kushuhudia pambano lake na Manny Pacquiao ifikapo tarehe mbili mwezi wa tano mwaka huu ambapo pambano hilo limepangwa kufanyika.

Mayweather ambae anarekodi ya kushinda mapambano yake yote 47 amemwambia mpinzani wake Pacquiao kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Los Angeles siku ya jumatano kuwa hakuwa tayari kukubali kushindwa.

Pacquiao pia kwa upande wake mapema alisema kuwa atampiga bondia huyo bora wa Amerika anaesifika kwa ubora kwenye mchezo wa masumbwi.

Mpiganaji huyo raia wa Ufilipino anarekodi ya kushinda mapambano 57, sare mbili na kushindwa mara tano kwenye mapambano yake

Tarehe mbili mwezi wa tano dunia itasimama kushuhudia pambano kubwa lakihistoria alisema Mayweather

kupitia mtandao wa twitter pia Mfilipino huyu alindika amejitoa ili kuthibitisha kuwa atamshinda bondia asiepigika

_81585294_pacquiao_twitter

 

Comments are closed.