GARISSA: WANAFUNZI WAREJEA CHUONI

GARISSA: WANAFUNZI WAREJEA CHUONI

Like
233
0
Monday, 11 January 2016
Local News

WANAFUNZI wamerejea tena katika Chuo Kikuu cha Garissa na kuanza masomo miezi tisa baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na shambulio la al-Shabab, Nchini Kenya.

Serikali imesema imeweka usalama wa kutosha kuhakikisha kundi hilo kutoka Somalia haliwezi likashambulia tena, lakini licha ya hakikisho kutoka kwa maafisa wa usalama, ni wanafunzi wachache pekee waliorejea chuoni.

Takriban wanafunzi 800 wa kufadhiliwa na serikali, waliokuwa wakisomea katika chuo hicho kabla ya shambulio kutokea, walihamishiwa chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret.

Comments are closed.