GAZA: MAJESHI YA HAMAS YALAUMIWA KWA UKATILI

GAZA: MAJESHI YA HAMAS YALAUMIWA KWA UKATILI

Like
233
0
Wednesday, 27 May 2015
Global News

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo ya mpakani.

Mashambulizi hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kwa kushirikiana na Israel.

Amnesty imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu wa Gaza, Hamas wao wanatumia fursa hiyo kujipanga kwa ushindi.

Comments are closed.