GHANA: MAJAJI 34 KUCHUNGUZWA KWA KULA RUSHWA

GHANA: MAJAJI 34 KUCHUNGUZWA KWA KULA RUSHWA

Like
205
0
Thursday, 10 September 2015
Global News

UCHUNGUZI uliofanywa Nchini Ghana, na mwandishi habari za uchunguzi , Anas Aremeyaw Anas uliomchukua miaka miwili umegundua kuwa majaji pamoja na viongozi wa juu wa mahakama nchini humo wanakula rushwa .

Anas tayari amekwisha waandikia waraka Rais wa nchi hiyo pamoja jaji mkuu ambao nao tayari wamekwisha andaa tume ya kuwahoji majaji wote wanaotuhumiwa.

Anes, Mwandishi wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwanasheshia aliwafuata majaji kuwapa hongo ili wawaachie huru watuhumiwa. Katika maeneo mengine alijifanya mwenye kushitaki ili atoe hongo. Leo, chombo kinachohusika na kuwaadhibu wanasheria wanaolalamikiwa kwa rushwa kitawasikiliza majaji wote 34 wanaohusishwa na kashifa hiyo.

Comments are closed.