GHANA: MAJAJI 34 MASHAKANI

GHANA: MAJAJI 34 MASHAKANI

Like
190
0
Tuesday, 15 September 2015
Global News

JAJI mkuu wa Ghana . Georgina Theodora Wood amehutubia nchi kuhusu kashifa kubwa ya rushwa dhidi ya majaji na kuahidi kuchukua hatua na maamuzi ya haraka kuhusu madai dhdi ya majaji 34 wanaoshukiwa na kashifa hiyo. Hii ni mara ya kwanza tangu taarifa ya kashifa hiyo kutokea hali iliyosababisha Jaji huyo mkuu kuzungumza hadharani ambapo amesema kuwa idara ya sheria inapitia katika kipindi kigumu kutokana na maadili ya kisheria yaliyowekwa na wakongwe wa sheria kutetereka. Jaji huyo mkuu amesema kuwa uchunguzi huo uliofanywa hivi karibuni kuhusu kesi zaidi ya tatu umesaidia kuwaachisha kazi majaji watatu wa makahama kuu na idadi kubwa ya wafanyakazi wa Idara hiyo ya sheria.

Comments are closed.