GHASIA KENYA: CHUO CHAFUNGWA

GHASIA KENYA: CHUO CHAFUNGWA

Like
206
0
Tuesday, 13 October 2015
Global News

CHUO kikuu kimoja nchini Kenya kimefungwa baada ya mwanafunzi mmoja kufariki wakati wa makabiliano kati ya wanafunzi na polisi usiku wa jana.

Kaimu Naibu Chansela wa chuo kikuu hicho cha Maseno Bi Catherine Muhoma, ameagiza chuo hicho kufungwa haraka kutokana na vurugu kuzidi.

Ghasia zilianza baada ya polisi kudaiwa kulifyatulia risasi gari lililokuwa likitumiwa na wanafunzi kupigia debe mmoja wa wagombea katika kampeni za uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi chuoni.

Comments are closed.