Godbless Lema azungumza na waandishi kuhusu Mo Dewji

Godbless Lema azungumza na waandishi kuhusu Mo Dewji

Like
982
0
Tuesday, 16 October 2018
Local News

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kujiuzulu kutokana na matukio ya utekaji yanayojitokeza nchini ikiwemo la mfanyabiashara ‘Mo Dewji’. Akizungumza na wanahabari leo Oktoba 16, Lema amesema kuwa kitendo cha waziri Lugola kuzuia watu kuzungumzia matukio ya utekwaji wa watu yanayojitokeza kwa sasa hapaswi kufanya hivyo badala yake ni kung’atuka ili kupisha kashfa.
Lema amesema kuwa serikali inatakiwa kuviruhusu vyombo vya ulinzi vya kimataifa kuisaidia Tanzania na kuchunguza mfululizo wa matukio hayo yakiwemo ya kushambuliwa kwa Lissu na kupotea kwa mwanahabari.
“Waziri wa mambo ya ndani kakiri kwamba utekaji umekuwepo, na kuna watu wametekwa, na kuna watu wametoweka, ukiwa na hekima unang’atuka, tunaitaka serikali ifanye kila liwezekanalo mara moja kuhakikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa vinatupatia msaada kwenye hili haraka iwezekanavyo”, amesema Lema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *