GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY KUMUOMBEA RAIS KIKWETE

GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY KUMUOMBEA RAIS KIKWETE

Like
314
0
Thursday, 13 November 2014
Local News

HUDUMA ya Good News For all Ministry ya Jijini Dar es salaam imetoa wito kwa wananchi wote nchini kuhudhuria  maombezi ya kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE yatakayofanyika kesho ili afya yake iweze kuimarika na kurejea nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa Habari Njema kwa Wote Askofu CHARLES GADI ameeleza kuwa Maombezi hayo yatafanyika Mpinga Bagamoyo na yanatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi  wa Dini zote sanjari na Viongozi wa Kitaifa na Serikali.

Mbali na hayo GADI amebainisha kuwa kama Kiongozi wa Dini anawaomba Watanzania kuchangia  fedha ili iweze kununua ndege ya kumuhudumia  Rais pindi apatapo dharura na amewasisitiza wananchi watakaoshindwa kuhudhuria maombezi  ni vyema washirikiane nao kwa kufunga na kuomba popote walipo.

 

Comments are closed.