GPSA KUSIMAMIA MFUMO WA UDHIBITI WA MAFUTA KATIKA VISIMA NA MAGARI YA SERIKALI

GPSA KUSIMAMIA MFUMO WA UDHIBITI WA MAFUTA KATIKA VISIMA NA MAGARI YA SERIKALI

Like
427
0
Wednesday, 12 August 2015
Local News

KUTOKANA na umuhimu na wingi wa Matumizi ya Mafuta kwenye Magari na Mitambo ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na gharama kubwa wakala wa huduma ya ununuzi serikalini GPSA umeamua kusimamia mfumo wa udhibiti wa mafuta katika visima na magari ya serikali.

 

Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa  huduma hiyo NAFTAL SINGWEJO amesema  kuwa lengo kubwa la mfumo huo ni kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa matumizi ya mafuta ambao utapunguza gharama za ununuzi na matumizi ya magari hayo.

Comments are closed.