ZAIDI ya watu 130 wamefariki dunia baada ya maporomoko ya matope kukiangamiza kijiji kimoja, kando ya mji mkuu wa Guatemala.
Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka za nchi hiyo ya Amerika ya Kati, ikiwa ni siku ya tatu tangu janga hilo kutokea, zinasema idadi mpya ya waliopatikana wamekufa imefikia 131, huku wengine 300 wakiwa hawajuilikani walipo.
Maporomoko yenye matope mazito yalikifunika kijiji cha El Cambray katika manispaa ya Santa Cantarina Pinula, na kuharibu nyumba 125, usiku wa Alhamisi.