GUINEA: MGONJWA WA MWISHO WA EBOLA APONA NA KURUHUSIWA

GUINEA: MGONJWA WA MWISHO WA EBOLA APONA NA KURUHUSIWA

Like
260
0
Tuesday, 17 November 2015
Global News

MAAFISA wa Afya nchini Guinea wamesema mgonjwa wa mwisho aliyeripotiwa kupata maradhi ya Ebola amepona na ameruhusiwa kutoka kwenye kituo cha matibabu kilichopo mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry.

Ugonjwa huo ulioanza nchini Guinea, umeua zaidi ya watu 11,000 Afrika magharibi ingawa tayari Nchi jirani za Sierra Leone na Liberia zimefanikiwa kuutokomeza ugonjwa huo.

Mgonjwa mmoja aliyekuwa amebaki ni mtoto wa siku 19 ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa huo huku msemaji wa kitengo kinachoratibu mapambano dhidi ya Ebola amesema vipimo vilivyochukuliwa mara mbili vimethibitisha kuwa mtoto huyo amepona.

Comments are closed.