GWAJIMA AKANUSHA TAARIFA ZA DR SLAA

GWAJIMA AKANUSHA TAARIFA ZA DR SLAA

Like
269
0
Tuesday, 08 September 2015
Local News

ASKOFU Mkuu wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amekanusha taarifa zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo-CHADEMA-dokta Wilbroad SLaa kuwa yeye alimpa taarifa kwamba maaskofu 30 wa kanisa katoliki walipewa fedha na mgombea urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi ukawa mheshimiwa Edward Lowasa ili wamuunge mkono katika harakati zake.

Askofu Gwajima ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa hizo ambapo amesema kuwa habari iliyotolewa na dokta Slaa juu yake sio ya kweli kwani ina lengo la kuwadharirisha viongozi hao wa dini.

Kuhusu suala la mheshimiwa Lowasa kuhamia chadema Askofu Gwajima amesema kuwa yeye hakumfuata dokta Slaa isipokuwa dokta Slaa ndiye aliyemfuata na kumwomba amuunganishe na kiongozi huyo wa siasa ili ajiunge nao na wafanye kazi pamoja.

Comments are closed.