GWAJIMA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

GWAJIMA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Like
311
0
Thursday, 10 September 2015
Local News

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi zinazomkabili zitakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi ya kwanza ambayo inamkabili Gwajima peke yake, anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo kunatokana na upelelezi wa kesi hiyo kukamilika na mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Comments are closed.