HAKI ZA BINADAMU: OBAMA AIONYA ETHIOPIA

HAKI ZA BINADAMU: OBAMA AIONYA ETHIOPIA

Like
138
0
Monday, 27 July 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika.

Kwa upande wake Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.

 

Comments are closed.