HALI BADO TETE UKRAINE KUFUATIA ONGEZEKO LA MASHAMBULIZI DHIDI YA RAIA

HALI BADO TETE UKRAINE KUFUATIA ONGEZEKO LA MASHAMBULIZI DHIDI YA RAIA

Like
260
0
Thursday, 05 February 2015
Global News

SHIRIKA linalojihusisha na maswala ya usalama na ushirikiano barani Ulaya-OSCE limesema hali ya Mashariki ya Ukraine inazidi kuwa mbaya na mashambulizi dhidi ya Raia yanazidi kuongezeka.

Msemaji wa Shirika hilo amesema wanafuatilia hali ilivyo nchini Ukraine na kwamba silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zilitumika juma lililopta katika mji unaoshikiliwa na waasi .

Baadae hii leo, Mkuu wa Shirika la OSCE atahutubia Baraza lake la kudumu, ambapo anatarajiwa kutoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda katika Mji unaodhibitiwa na Serikali wa Debaltseve ambao mapigano yameongezeka Wiki za hivi karibuni.

Comments are closed.