HALI BADO TETE UKRAINE LICHA YA MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPAMBANO

HALI BADO TETE UKRAINE LICHA YA MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPAMBANO

Like
298
0
Monday, 16 February 2015
Global News

WANADIPLOMASIA wamesema Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa watakuwa na mashauriano zaidi juu ya usitishaji mapigano Mashariki mwa Ukraine, lakini bado hawapo tayari kupitisha maazimio.

Baraza hilo la Amani na Usalama Duniani linatarajiwa kupiga kura juu ya rasimu ya maazimio dhidi ya Urusi inayotaka pande zote kutekeleza mpango uliotoa nafasi ya kusitishwa kwa mapigano kulikoanza siku ya Jumapili.

Licha ya makubaliano hayo, milio ya mizinga imekuwa ikisikika Mashariki mwa Ukraine.

Comments are closed.