HALI YA MIFUMO YA VYOO DAR NI HATARI

HALI YA MIFUMO YA VYOO DAR NI HATARI

Like
214
0
Thursday, 19 March 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa licha ya kuwa na mazingira duni ya vyoo jijini karibia  asilimia 99 ya wakazi wa Dar es salaam  wana vyoo lakini ni asilimia 10 tu ya wakazi hao ambao vyoo vyao vimeunganishwa na mfumo wa kupitisha au kutoa maji taka.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano uliokutanisha serikali, wadau, Taasisi na Asasi za kiraia kujadili hali halisi ya masuala ya usafi wa mazingira ya vyoo na kuangalia hali ya mtandao wa maji taka na njia za kutatua changamoto hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Meneja programu kutoka Asasi ya Kiraia ya CCI,  Mwanakombo Mkanga amesema  mjadala umejikita zaidi katika utafiti unaohusu maswala ya vyoo katika maeneo ya makazi yasiyopimwa.

 

Comments are closed.