HALI YA TAHADHARI KUENDELEZWA BRUSSELS

HALI YA TAHADHARI KUENDELEZWA BRUSSELS

Like
189
0
Tuesday, 24 November 2015
Global News

WAZIRI Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amesema hali ya tahadhari itaendelea kubaki kwa kiwango cha juu katika mji wa Brussels.

Waziri huyo amesema wasiwasi wa tishio la ushambulizi kama lililowahi kutokea siku kumi zilizopita mjini Paris bado ni mkubwa ingawa kuanzia Jumatano shule zitafunguliwa na usafiri wa treni katika mji mkuu utakuwepo.

Mamlaka ya Ubelgiji imesema hadi sasa inawashitaki watuhumiwa wanne kwa kujihusisha katika shughuli zinazohusiana na ugaidi.

Comments are closed.