HALI YA WASIWASI YAANZA KUTANDA BURUNDI

HALI YA WASIWASI YAANZA KUTANDA BURUNDI

Like
230
0
Monday, 03 August 2015
Global News

KUMERIPOTIWA kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini Burundi kufuatia mauaji ya Jenerali mmoja ambaye alikuwa mtu wa karibu ya Rais Pierre Nkurunzinza katika masuala ya kiusalama.

Jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa jana kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari katika mji mkuu Bujumbura.

Nshimirimana ambaye alikuwa mshauri mwandamizi wa masuala ya usalama wa Rais Pierre Nkurunzinza aliuawa wakati watu waliokuwa ndani ya gari walipomfyatulia risasi yeye na mlinzi wake katika kitongoji cha mji mkuu cha Kamenge.

Comments are closed.