HALI YA WASIWASI YATANDA BURKINA FASO

HALI YA WASIWASI YATANDA BURKINA FASO

Like
205
0
Thursday, 17 September 2015
Global News

WALINZI wa rais nchini Burkina Faso wamemkamata rais wa mpito Michel Kafando na waziri mkuu Isaac Zida na hivyo kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya wasiwasi wiki chache tu kabla uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani Blaise Compaore.

Kukamatwa kwao kulisababisha maandamano ya barabarani nje ya ikulu ya rais ambako viongozi hao walikuwa wakizuiliwa.

Milio ya risasi ilisikika wakati wanajeshi walipokuwa wakiwatawanya mamia ya waandamanaji na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameghadhabishwa na hatua hiyo na kutaka viongozi hao waachiwe mara moja akisema hatua hiyo inakiuka katiba ya Burkina Faso na mkataba wa utawala wa mpito.

Comments are closed.