HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUAJIRI MAAFISA HABARI

HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUAJIRI MAAFISA HABARI

Like
272
0
Wednesday, 06 April 2016
Local News

SERIKALI imeagiza kila mkoa na kila Halmashauri nchini kuajiri Maafisa wa Habari na kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao vyote vya maamuzi pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za maafisa habari ili kuboresha mawasiliano ndani ya serikali na mawasiliano ya serikali na umma.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nauye, wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Kigoma, aliyoifanya kwa ajili ya kutembelea idara zilizo chini ya wizara yake ambapo amekutana na wadau mbali mbali wa wizara hiyo.

 

Waziri Nape, ambaye pia amekabidhi iPad kwa maafisa habari wanne wa serikali waliopo mkoani Kigoma, amesema wengi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kwa sababu hawana taarifa kutokana na kutopewa kipaumbele cha kuhudhuria vikao vya maamuzi.

Comments are closed.