HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YAPEWA MWEZI MMOJA KUBOMOA JENGO REFU KATIKA MTAA WA INDIRAGHANDI

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YAPEWA MWEZI MMOJA KUBOMOA JENGO REFU KATIKA MTAA WA INDIRAGHANDI

Like
365
0
Tuesday, 26 January 2016
Local News

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lililojengwa chini ya kiwango katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia jana.

Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi ya kikazi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambapo huko pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta ya Ardhi.

Miongoni mwa changamoto alizozikuta ni pamoja na wananchi kuporwa viwanja vyao na kutakiwa kuchanga fedha ili kupewa sehemu ya viwanja hivyo hali iliyomlazimu, Waziri kuwaagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya kipindi cha miezi 6 wawe wamewapatia wananchi viwanja vyao.

Comments are closed.