Hatima  ya Nigeria Kuvuka Hatua ya  Makundi  Kujulikana Leo Dhidi ya Iceland

Hatima ya Nigeria Kuvuka Hatua ya Makundi Kujulikana Leo Dhidi ya Iceland

Like
514
0
Friday, 22 June 2018
Sports
Michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inaendelea kushika kasi tena ambapo Afrika itakuwa inawakilishwa na Nigeria itakayokuwa kibaruani dhidi ya Iceland.
Matumaini pekee ya Nigeria kuendelea kusalia kwenye michuano hiyo yataonekana leo endapo itaibuka na ushindi wa mabao mengi huku ikitegemea matokeo ya mechi zingine zilizosalia.
Timu hiyo ilipoteza mechi yake ya kwanza ilipocheza dhidi ya Croatia kwa kufungwa mabao 2-0.
Msimamo kundi D unaonesha imeshikilia mkia namba 4 ikiwa haina alama yoyote huku Iceland na Argentina wakiwa na pointi moja kwa kila timu wakati Croatia wakiwa na 6.
Mechi hii itaanza majira ya saa 12 kamili jioni huku mapema saa 9 Brazil wataanza kukipiga na Costa Rica na saa 3 usiku Serbia watakuwa wanacheza na Switzerland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *