HATMA YA KESI YA UMBALI KWA WAPIGA KURA KUFAHAMIKA LEO

HATMA YA KESI YA UMBALI KWA WAPIGA KURA KUFAHAMIKA LEO

Like
188
0
Thursday, 22 October 2015
Local News

KESI ya Kikatiba kuhusu tafsiri ya Umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya Kupiga kura Wakati wa Uchaguzi mkuu inasomwa leo na kutolewa maelekezo maalum baada ya hapo jana kuahirishwa.

Akizungumza jana wakati anatoa maamuzi hayo mwenyekiti wa jopo la majaji wanaosikiliza  kesi hiyo JAJI SAKIETI KIHIYO  ameleza kuwa  baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili kuhusiana kesi hiyo jana, mahakama  imetoa uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo watatoa maamuzi yenye maelekezo maalum kuhusu umbali ambao wapiga kura watatakiwa wakae baada ya kupiga kura siku ya Uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Comments are closed.