HELIKOPTA YA JESHI LA AFGHANISTAN YAANGUKA ZABUL

HELIKOPTA YA JESHI LA AFGHANISTAN YAANGUKA ZABUL

Like
222
0
Thursday, 06 August 2015
Global News

HELIKOPTA  ya  jeshi  la  Afghanistan  imeanguka  katika jimbo  la  kusini  la  Zabul  leo, na  wanajeshi  17 wameuwawa, ikiwa  ni  pamoja  na  marubani watano.

Mkuu  wa  polisi  wa  jimbo  hilo Mirwais  Noorzai  amesema sababu  ya   kuanguka  helikpota  hiyo  haifahamiki  na uchunguzi  unafanyika.

Wizara  ya  ulinzi  imesema  ajali hiyo  inaaminika  imesababishwa  na  hitilafu  ya  kiufundi , lakini  hayakutolewa  maelezo  zaidi.

 

Comments are closed.