HILLARY CLINTON amejitangazia rasmi ushindi kwenye kura za mchujo za chama chake cha Democratic baada ya kushinda majimbo kadhaa muhimu kwenye chaguzi za jana na hivyo kujiimarishia nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kwanza mwanamke wa urais wa Marekani.
Hata hivyo mpinzani wake, Bernie Sanders, amekataa kujitoa kwenye kinyang’anyironi na badala yake ameapa kusonga mbele hadi dakika za mwisho.
Kwa upande mwengine, mgombea mteule wa chama cha Republican, Donald Trump, amejizolea ushindi mkubwa kwenye majimbo ya New Mexico, New Jersey, North Dakota na Montana.