MGOMBEA urais wa Marekani anayeongoza katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amekataa kushiriki mdahalo wa nne dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders.
Maafisa wake wa kampeni wamesema, Bi Clinton ameamua kuwa ni vyema kutoshiriki mdahalo huo na badala yake akabiliane na mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump.
Awali Bi. Clinton alikuwa amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.