HOFU YA KUZUKA KWA EBOLA DRC YATANDA

HOFU YA KUZUKA KWA EBOLA DRC YATANDA

Like
231
0
Friday, 03 July 2015
Global News

JUMLA ya watu wanne wamefariki dunia wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mbali na kutokea kwa taarifa za mgonjwa huyo wa Ebola Mamlaka za Afya nchini humo zimesema kuwa bado zinachunguza uwezekano wa kutokea zaidi kwa mlipuko wa ugonjwa huo.

Waziri wa Afya Felix Kabange amesema wafanyakazi wa afya wamepelekwa katika kijiji cha Masambio kilichoko kilomita 270 kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo wawindaji sita walipatwa na homa Ijumaa iliyopita wakiwa na dalili za ugonjwa huo baada ya kuua na kula nyama ya Paa.

Comments are closed.