HOFU YA KUZUKA KWA EBOLA YATANDA NIGERIA

HOFU YA KUZUKA KWA EBOLA YATANDA NIGERIA

Like
189
0
Friday, 09 October 2015
Global News

WASIWASI umezuka katika mji wa Calabar, kusini mwa Nigeria kutokana na mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazofanana na zile za ugonjwa wa Ebola.

Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo limesema kuwa watu kumi wamewekwa karantini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia, zimefanikiwa kukaa wiki moja bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka 2014.

Comments are closed.