HOFU YATANDA MAREKANI BAADA YA EBOLA KUINGIA NEWYORK

HOFU YATANDA MAREKANI BAADA YA EBOLA KUINGIA NEWYORK

Like
340
0
Friday, 24 October 2014
Global News

Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali  ya Bellevue mjini Newyork.

Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.

Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo.

Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.

ebolaaa22

picha ya mpenzi wa Dr Craig Spencer ambae nae pia amewekwa kwenye uangalizi maalum

ebolaaaa

Dr Craig Spencer

 

 

 

 

 

 

 

 

ebolaaahouse

polisi wakiwa kwenye nyumba ya Dr Craig Spencer

 

Comments are closed.