Huitaji elimu ya chuo kikuu kutambua hali ya Manchester United – Mournho

Huitaji elimu ya chuo kikuu kutambua hali ya Manchester United – Mournho

Like
409
0
Friday, 23 March 2018
Sports

Jose Mourinho

Kocha Mkuu wa klabu ya mashetani wekundu Manchester United, Jose Mourinho hapo jana amesema kuwa watu wenye akili na fikira za kuelewa na kuchambua mambo ya msingi wanatambua hali ya timu hiyo kwa sasa inavyopita kwenye kipindi cha mpito.

Mourinho ambaye ni raia wa Ureno mara kadhaa amekuwa akishtumiwa na mashabiki kwa namna ya mfumo wake wa uchezaji ambao unadaiwa kutokuwa na ubunifu.

Mashabiki wa United walizidisha shutuma zao zaidi mara baada ya klabu hiyo kutolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya na timu ya Sevilla katika dimba la Old Trafford.

Katika mazungumzo yake na chombo cha habari Mourinho amesema kuwa katika historia ya mchezo wa soka duniani kuna wakati klabu kubwa hupitia kipindi cha mpito.

“Katika historia ya mchezo wa soka duniani kote na wala sio Uingereza pekee kunawakati klabu kubwa hupitia katika kipindi kigumu cha mpito na zipo nyingine huwa zinakuwa na matokeo mazuri ya mfululizo”.     

Mpaka sasa klabu hiyo inashika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City kwa kuzidiwa pointi 16.

Comments are closed.