HUJUMA ZA BAADHI YA WAFANYABIASHARA ZAIGHARIMU SERIKALI

HUJUMA ZA BAADHI YA WAFANYABIASHARA ZAIGHARIMU SERIKALI

Like
196
0
Wednesday, 01 April 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa  hujuma zinazofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara nchini, zimeendelea kuigharimu Serikali kwa kuikosesha mapato.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya Wafanyabiashara hao kuingiza bidhaa ambazo, zimekuwa zikilipiwa Ushuru mdogo.

Kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na wimbi la Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam, ambapo huandikisha taarifa na maelezo tofauti na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena, ili kuwawezesha kukwepa kodi kwa kulipia kiasi kidogo.

Comments are closed.