HUKUMU YA KIFO KWA MAGAIDI KUREJESHWA PAKISTAN

HUKUMU YA KIFO KWA MAGAIDI KUREJESHWA PAKISTAN

Like
364
0
Wednesday, 17 December 2014
Global News

PAKISTAN imesema itaondoa marufuku ya kutolewa adhabu ya kifo katika kesi zinazohusiana na ugaidi.

Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa tangazo hilo leo, siku moja baada ya wapiganaji wa Taliban kuwaua watu 141 katika shambulizi lililofanyika kwenye shule moja inayoendeshwa na jeshi.

PAKI2

mmoja wa wanafunzi alienusurika katika shambulio hilo

Shambulizi hilo la kigaidi lililofanyika kwenye mji wa Peshawar, ni baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Pakistan. Hukumu za kifo ziko katika amri za kitabu cha Pakistan na majaji wameendelea kutoa adhabu hiyo, lakini amri ya kusitisha adhabu ya mauaji kwa raia imekuwa ikiheshimiwa tangu mwaka 2008.

 

 

Comments are closed.