ICC: NTAGANDA AKANUSHA MASHTAKA YA UHALIFU WA KIVITA

ICC: NTAGANDA AKANUSHA MASHTAKA YA UHALIFU WA KIVITA

Like
241
0
Wednesday, 02 September 2015
Global News

ALIYEKUWA kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, amekanusha mashtaka aliyokuwa yakimkabili ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadam, baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kimataifa ya jinai, ICC, iliyoko mjini the Haque leo.

Ntaganda anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya raia mia nane na kuwabaka watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini kama watumwa wa ngono.

Mashtaka yote yanahusiana na wakati alipokuwa akiongoza mapigano katika eneo la Ituri Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka wa 2002 na 2003.

Comments are closed.