Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Reykjavik kukaribisha msafara wa timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani ulaya mwaka huu 2016.
Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya basi kubwa la wazi wakisindikizwa na ngoma hadi katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki waliwasalimia kwa shangwe na makofi .
Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa ya Kombe la mataifa barani Ulaya ilifikia ukingoni mwa mashindano mwaka huu baada ya kupata kichapo kutoka kwa Ufaransa kwa magoli 5 – 2.
Hata hivyo kabla ya kuondolewa ilionyesha maajabu pale ilipoiondoa England kwenye hatua ya kumi na sita bora.