IDADI YA WANAWAKE WANAOFARIKI WAKATI WA KUJIFUNGUA YAZIDI AFRIKA MAGHARIBI

IDADI YA WANAWAKE WANAOFARIKI WAKATI WA KUJIFUNGUA YAZIDI AFRIKA MAGHARIBI

Like
341
0
Tuesday, 11 November 2014
Global News

IDADI ya wanawake wanaofariki wakati wa kujifungua katika nchi za magharibi mwa Afrika zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola inazidi kupanda huku mwanamke mmoja kati ya saba katika nchi hizo akiwa katika hatari ya kufa kutokana na kutopokea usaidizi wakati wa kujifungua, watu wakihofia kuambukizwa Ebola kwa kushika damu na maji maji ya miili ya wajawazito.

Mashirika ya kutoa misaada 13 kutoka Uingereza yakiwemo Save the children,Action Aid na hata shirika la umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu yanakisia kuwa kiasi ya wanawake laki nane nchini Guinea,Sierra Leone na Liberia wanatarajiwa kujifungua katika kipindi cha miezi kumi na miwili ijayo na 120,000 kati yao huenda wakakabiliwa na matatizo wakati wa kujifungua.

Ebola imewaua kiasi ya watu 5,000 katika nchi hizo tatu za magharibi mwa Afrika.

Comments are closed.