IDADI YA WATAHINIWA KIDATO CHA NNE YAONGEZEKA MBEYA

IDADI YA WATAHINIWA KIDATO CHA NNE YAONGEZEKA MBEYA

Like
459
0
Wednesday, 28 October 2015
Local News

JUMLA ya watahiniwa 12,011 wa kidato cha nne Jijini Mbeya wanatarajiwa kuanza mtihani wa Taifa Novemba mbili mwaka huu, ikilinganishwa na wanafunzi 2,895 waliofanya mtihani huo mwaka jana.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa halmashauri ya jiji la Mbeya kwa niaba ya Afisa Elimu sekondari Jaquline Msuya amesema kati ya watahiniwa hao wasichana ni 6373 na wavulana 5638.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondari ya Southern Highland ya jijini Mbeya Chamila Evarist amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanafunzi wote waliosajiliwa wanafanya mtihani huo wa Taifa.

Comments are closed.