IDADI ya watu wanaosumbuliwa na njaa ulimwenguni imepungua na kufikia chini ya watu milioni 800-kwa mara ya kwanza tangu Umoja wa mataifa ulipoanza kutoa takwimu hizo.
Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo-FAO ambalo limesema katika ripoti yake ya mwaka iliyochapishwa jana.
Shirika hilo lenye makao yake mjini Rome Italy limesema kuna watu milioni 795 ulimwenguni wanaosumbuliwa na njaa-idadi hiyo ikiwa na upungufu wa watu milioni 216 ikilinganishwa na jinsi hali namna ilivyokuwa kati ya mwaka 1990-hadi 1992.