IDADI YA WAZAZI WANAOTUPA WATOTO YAPUNGUA

IDADI YA WAZAZI WANAOTUPA WATOTO YAPUNGUA

Like
300
0
Friday, 13 November 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa idadi ya wazazi ambao hutupa watoto wao imepungua kwa kasi tofauti na elimu ambayo hutolewa na serikali, jeshi la polisi pamoja na wadau mbalimbali wa haki za watoto juu ya kuwatunza watoto.

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa IRINGA–ACP- RAMADHAN MUNGI wakati akizungumza na wadau mbalimbali juu ya suala hilo na kuwaonya wazazi wenye tabia ya kutupa watoto mara baada ya kujigungua kuacha haraka kwani kufanya hivvo, ni kwenda kinyume na sheria za haki za binadamu.

Aidha kamanda Mungi amekemea vikali tabia ya ukatili kwa watoto unaofanywa na baadhi ya watu ikiwemo kuwabaka na hata kuwalawiti kwani ni vitendo vya udhalilishaji.

 

Comments are closed.