IDARA ya Uhamiaji nchini imetoa wito kwa Wamiliki wa Viwanda na Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutafuta namna nzuri ya kutunza mazingira kwa kuangalia njia mbadala ya kuhifadhi vifaa vilivyokwisha kutumika.
Akizungumza na wadau mbalimbali katika Semina ya mazingira Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na fedha PANIEL MGONJA amesema lengo la Semina hiyo ni kuonyesha muongozo wa namna nzuri ya kutunza mazingira.
MGONJA amesema kuwa wao kama taasisi ya Uhamiaji wameamua kutekeleza sheria ya Mazingira kwa kuhakikisha Majengo na Nyumba za makazi zinakuwa katika hali ya kutunza Mazingira kwa faida ya nchi na wananchi.