IDLIB: 30 WAHOFIWA KUFA KWA MASHAMBULIZI YA NDEGE KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI

IDLIB: 30 WAHOFIWA KUFA KWA MASHAMBULIZI YA NDEGE KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI

Like
234
0
Friday, 06 May 2016
Global News

AFISA mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema mashambulizi ya ndege za angani katika kambi ya wakimbizi,yanahofiwa kuwaua zaidi ya watu 30.

Mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika umoja wa mataifa, Stephen O’Brien ametaka pawepo uchunguzi juu ya shambulizi hilo lililotokea katika jimbo la Idlib, karibu na mpaka wa Uturuki.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond amemtuhumu Rais wa Syria Bashar Al-Assad kwa kuonyesha dharau juu ya juhudi za kimataifa kumaliza mapigano nchini humo.

Comments are closed.