IGUNGA: KAYA ELFU 18 KUNUFAIKA NA MPANGO WA RUZUKU ZA PEMBEJEO

IGUNGA: KAYA ELFU 18 KUNUFAIKA NA MPANGO WA RUZUKU ZA PEMBEJEO

Like
437
0
Tuesday, 01 December 2015
Local News

ZAIDI ya kaya Elfu 18 katika kata nane za Halmashauri ya wilaya ya IGUNGA mkoani Tabora zitanufaika na mpango wa ruzuku za pembejeo katika msimu huu wa mwaka 2015-2016.

Afisa Maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Igunga, Hossea Samaruku ameeleza hayo wakati akizungumzia hali halisi ya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku katika wilaya hiyo.

Samaruku amesema vijiji 43 vya wilaya hiyo vitashiriki kutekeleza mpango huo na kata zitakazonufaika na ruzuku ni pamoja na Nyandekwa, Nkinga na Igoweko.

Comments are closed.