IKULU YA URUSI YAISHUTUMU MAREKANI KUVURUGA AMANI SYRIA

IKULU YA URUSI YAISHUTUMU MAREKANI KUVURUGA AMANI SYRIA

Like
286
0
Tuesday, 04 August 2015
Global News

IKULU ya Urusi Kremlin, inasema hujuma za ndege za kivita za Marekani dhidi ya vikosi vya serikali ya Syria zinaweza kuvuruga zaidi utulivu nchini humo na kuwafaidisha wanamgambo wa itikadi kali wa Dola ya Kiislam – IS.

Matamshi hayo ya Urusi yametolewa kufuatia ripoti iliyotolewa na gazeti mojawapo nchini humo inayosema serikali ya Marekani mjini Washington inapanga kutumia ndege za kivita kufanya hujuma nchini Syria ili kuwasaidia makuruti wanaopambana dhidi ya Dola la Kiislam.

Hata hivyo amebainisha kuwa hujuma kama hizo zinaweza kulenga jeshi la Syria, sawa na kundi linalofungamana na Al-Qaida na makundi kadhaa mengine kama hilo hali inayoweza kupoteza uwezo wa kukabiliana na kuenea kwa kundi hilo.

 

Comments are closed.