IKULU YAKANUSHA KUTOA RATIBA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU

IKULU YAKANUSHA KUTOA RATIBA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU

Like
389
0
Wednesday, 25 November 2015
Local News

OFISI ya Rais Ikulu, imekanusha taarifa zilizoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya rais Ikulu, imetoa ratiba ya maadhimisho ya siku ya Uhuru Tarehe 9 Disemba 2015.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya rais, imeeleza kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuwataka wananchi wazipuuze.

Tayari Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue ameshatoa maelekezo kwa viongozi wa mikoa na Wilaya zote juu ya namna bora ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli.

Comments are closed.