INDIA: 23 WAPOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA DARAJA

INDIA: 23 WAPOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA DARAJA

Like
188
0
Friday, 01 April 2016
Global News

MAMIA ya waokoaji wakiongozwa na majeshi, wahandisi na matabibu wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha katika mji wa India wa Calcutta kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye barabara ya juu iliyoanguka wakati ikijengwa.

Maafisa wanasema hadi sasa watu 23 wamekufa na mamia kujeruhuwa na wengine wakiwa bado wamefukiwa na kifusi.

Inasadikiwa watu wengi wamefukiwa ambapo hadi sasa tayari watu 23 wamethibitishwa kufariki na mamia wengine kujeruhiwa ambao wanapatiwa matibabu.

Comments are closed.