IRAN YAIMARISHA ULINZI DHIDI YA URUSI

IRAN YAIMARISHA ULINZI DHIDI YA URUSI

Like
351
0
Monday, 09 November 2015
Global News

IMEELEZWA kuwa nchi ya Iran imenunua silaha kali ya ulinzi dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi ikiwemo Mtambo wa S-300 wenye uwezo wa kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300.

Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya makubaliano kama hayo na Iran ambapo Mwaka wa 2007 mataifa hayo yalikubaliana kuhusiana na mitambo hiyo ya ulinzi wa anga lakini walisitisha utekelezaji wake kufuatia marufuku iliyowekewa Iran kutokana na mipango yake ya kumiliki silaha za nyuklia.

Mtambo huo wa S-300 ulitumika kwa mara ya kwanza wakati wa vita baridi na ulionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabili ndege zaidi ya moja na makombora kwa umbali wa kilomita 300.

                                                 

Comments are closed.